Swali 176: Ni ipi hukumu ya kuwashambulia watawalii na waliokuja kutembelea miji ya Kiislamu?

Jibu: Kitendo hichi hakijuzu kumshambulia yeyote. Ni mamoja mtu huyo ni mtalii au mfanyakazi. Kwa sababu watu hao wamepewa amani. Wameingia kwa mkataba. Kwa hivyo haijuzu kuwashambulia. Lakini unachotakiwa ni kuinasihi nchi ili wazuie yale wanayoonyesha yasiyostahiki. Ama kuwashambulia ni jambo lisilojuzu. Haifai kwao kumuua, kumdhuru au kumuudhi mtu mmojammoja. Ni juu yao kwenda kuwashtaki kwa watawala. Kwa sababu kuwashambulia ni kuwashambulia watu walioingia kwa mkataba. Kwa hivyo haijuzu kuwashambulia. Lakini mtu anatakiwa apeleke jambo lao kwa wale wawezao kuwazuia kuingia au kuwakataza kuonyesha maovu hayo.

Kuhusu kuwanasihi, kuwalingania katika Uislamu au kuacha maovu – ikiwa ni waislamu – ni jambo linalotakikana na linasapotiwa na dalili za Kishari´ah. Allaah ndiye aombwaye msaada.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 363
  • Imechapishwa: 05/01/2020