Kusengenya dhambi kubwa au ndogo?  

Usengenyaji ni haramu. Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa ni dhambi kubwa. Amesema (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ

“Na wala wasisengenyane baadhi yenu wengineo. Je, anapenda mmoja wenu kula nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo!” (49:12)

Kundi la wanachuoni limesema ya kwamba pale alipofananisha usengenyaji ni sawa na kula nyama ya maiti, ni dalili ambayo imeonesha kuwa ni dhambi kubwa. Kwa kuwa imechofananishwa nacho ni kitu kikubwa. Kwa hivyo kilichofananishwa kinachukua hukumu ya kilichofananizwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 412
  • Imechapishwa: 14/05/2020