Kusemwe nini juu ya mtawala huyu?


Swali 106: Ni ipi hukumu ya Kishari´ah juu ya mtawala ambaye anahukumu kwa kanuni za kifaransa pamoja na kuzingatia kwamba anadai Uislamu, anaswali, anafunga na anahiji. Kusemwe nini juu yake?

Jibu: Ikiwa anaamini kuwa inajuzu kuhukumu kwa kanuni za kifaransa basi ni kafiri. Hapa ni pale ambapo ataona kuwa inaafaa kwake kufanya hivo. Ama akiwa haitakidi hivi au akawa na utata, basi ni lazima kumsimamishia hoja. Wako wanachuoni wenye kuona kwamba akibadilisha dini katika mambo yote ya nchi basi anakuwa kafiri kwa sababu ameibadilisha dini. Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amechagua maoni haya katika “Tafsiyr” yake na Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake “Tahkiym al-Qawaaniyn”. Amesema akibadilisha dini yote katika mambo yote yanayohusu nchi na si katika baadhi ya mambo tu. Hivyo anakuwa kafiri kwa sababu ameibadili dini. Wako wengine wanaosema kwamba ni lazima kumsimamishia hoja. Kwa sababu anaweza kuwa mjinga na anaweza kuwa na utata. Shaykh wetu ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) amechagua maoni haya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 275
  • Imechapishwa: 17/11/2019