Swali: Je, inajuzu kusema uongo kwa kukhofia kusibiwa na kijicho?

Jibu: Hapana, haijuzu. Uongo ni haramu. Kuhusu kufikwa na kijicho, amtegemee Allaah na hakuna kitachomdhuru. Akithirishe nyuradi na Dhikr. Hakuna kitachomdhuru kwa idhini ya Allaah. Vilevile aombe kinga kwa Allaah. Hakuna kitachomdhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (71) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-06-13.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020