Kusema Takbiyr mara ya pili ili waswaliji waweze kusikia

Swali: Niliswalisha nikiwa imamu na nikasahau kuleta Takbiyr kwa sauti nilipoenda katika Rukuu´. Niliisema kwa sauti ya chini. Nikakumbuka kuwa mimi ni imamu ambapo nikairudi mara ya pili kwa sauti ilihali nimerukuu. Baada ya Tasliym nikasujudu Sujuud ya kusahau. Nimefanya sawa?

Jibu: Ikiwa umeisema kwa sauti ili maamuma waweze kusikia, ni sawa. Haikuwa ni wajibu kwako kufanya Sujuud ya kusahau. Lililo wajibu kwako ni wewe maimamu wakusikie ili waweze kurukuu pamoja na wewe. Umefanya wajibu wako na hivyo haikuwa ni wajibu kwako kufanya Sujuud ya kusahau. Ni katika utimilifu wa uongozi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 21/12/2016