Kusema “Ni yuu yangu talaka”, “ni haramu juu yangu”

Swali: Baadhi ya watu wanachukulia sahali kwa neno: “Ni Haramu juu yangu”, au “Ni juu yangu Talaka”. Ni ipi hukumu ya maneno haya?

Jibu: Kwa kiasi atakavyokuwa amekusudia. Akisema: “Ni Haramu juu yangu” na akamkusudia mke wake, inakuwa ni Talaka. Kwa kuwa Talaka ni kuharamisha pia. Na ikiwa amekusudia yamini, inakuwa ni yamini. Na ikiwa amekusudia Talaka, inakuwa ni Talaka. Kwa kuwa ni katika Talaka ya kinaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/3269
  • Imechapishwa: 02/03/2018