Swali: Tumesikia kutoka kwa baadhi ya watuwazima kusini ya kwamba al-Khadhir bado yuhai na kwamba anapopita katika kijiji basi kijiji hicho kinapata kheri kama vile mvua na kheri nyenginezo. Ni vipi tutawarudisha katika usawa?

Jibu: Huu ni ukhurafi. Ikiwa kuna yeyote ambaye anaamini kwamba al-Khadhir ndiye ambaye analeta kheri, basi mtu huyo anakuwa ni mwenye kuabudu sanamu. Ninachotaka kusema ni kwamba huu ni ukhurafi. Usawa ni kwamba al-Khadhir kishakufa na hayupo. Yeye ni Mtume. Haiwezekani akawepo wakati  wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha asije kwake. Hili haliwezekani. Ikiwa kuna wenye kuamini ya kwamba anaenda katika mji na kwamba analeta kheri na mvua, hii ni imani ya kishirki. Ni lazima kuwafikishia na kuwabainishia ya kwamba imani hii ni ukhurafi na wala haina msingi wowote.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 06/12/2018