Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye amehifadhi sehemu katika Qur-aan kwa ajili ya selibasi ya masomo kisha baada ya matokeo ya mtihani hafuatilizi kile alichohifadhi na akaw amekisahau. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Naona kuwa uhalisia wa mambo ni kwamba mtu huyu amekhasirika na ameenda kinyume maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ipatilizeni Qur-aan. Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake inaponyoka haraka kuliko ngamia kwenye kamba yake.”

Nasema midhali Allaah amekuneemesha kuhifadhi kile kilichokusahilikia katika Qur-aan, basi akipatilize na airudirudi Qur-aan. Kwani:

“Hakika mbora wenu yule aliyejifunza Qur-aan na akawafunza wengine.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/903
  • Imechapishwa: 22/08/2018