Swali: Je, inajuzu kusafiri na Qur-aan kuipeleka katika nchi ya makafiri kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakataza kusafiri na Qur-aan katika ardhi (nchi) ya maadui?

Jibu: Haijuzu kusafiri kwenda na msahafu katika Bilaad-ul-Harb. Ama nchi iliyo na ahadi (mkataba) na Waislamu, hakuna neno kusafiri kwenda na msahafu na msahafu huu uwe mikononi mwa mwenye nao na asimpe kafiri. Haijuzu kumpa msahafu kafiri hata ikiwa ni katika nchi ya Waislamu. Kafiri anachoweza ni kusikilizishwa Qur-aan:

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

“Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah (Qur-aan).” (09:06)

Usimpe msahafu, sawa ikiwa ni katika nchi ya kikafiri au ya Kiislamu mpaka wakati ataposilimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (51) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-05-27.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014