Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya Hajj na ´Umrah pamoja na mfanya kazi  wa kike akiwa hana Mahram?

Jibu: Watu wa nyumbani wakihiji na wako na mfanya kazi wa kike asiyekuwa na Mahram, wahiji naye. Kwa sababu kuhiji pamoja naye kunamuhifadhi zaidi kuliko abaki nyumbani peke yake au kumwacha kwa mtu mwengine. Tunaona kuwa uende pamoja naye. Kwa sababu vinginevyo atabaki nyumbani peke yake bila ya Mahram.

Ama kuhusu kumtumia mwanamke bila Mahram mwanzoni nilikuwa nalichukulia wepesi fulani na nikisema kwamba akija na Mahram wake kisha Mahram huyo akarudi ni jambo la sahali. Lakini kumetokea matukio kutoka kwa baadhi ya watu wenye imani dhaifu na wasiozichunga heshima zao ambao wamenifanya mimi kusema hivi sasa: haifai kumtumia mfanya kazi wa kike isipokuwa awe pamoja na Mahram wake ambaye atabaki pamoja naye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1672