Usende msibani ambapo kuna mambo ya Bid´ah kama matanga

Swali: Mmoja katika ndugu au marafiki wa mtu akifa na wanaishi katika nchi nyingine, itafaa kwake kusafiri kwenda katika nchi hiyo wanayoishi ili kuwapa pole na kuwapoza juu ya kumpoteza kwao yule maiti au kitendo hicho kinazingatiwa ni kufunga safari ambako hakujuzu?

Jibu: Ikiwa ndani ya utoaji pole kuna Bid´ah na mambo ya kikhurafi, kama kwa mfano ufanywaji matanga ambao unafanywa katika baadhi ya miji, basi haifai kwao kushirikiana nao. Ni mamoja mtu huyo akasafiri au asisafiri. Kwa sababu kitendo hicho ni miongoni mwa Bid´ah na maovu. Kitendo hichi ni maovu. Hivyo haifai kwa mtu kwenda na kushiriki ndani yake. Ni mamoja iwe safari au kitu kingine. Ikiwa ni safari basi ni baya zaidi.

Ama ikiwa utoaji pole ni kuwapoza tu wale wafiliwa, kuzipoza hisia zao na kuwaombea msamaha na rehema wale maiti hakuna neno na khaswakhaswa ikiwa ni ndugu. Hakika kuna kheri kubwa katika kule kusafiri kwenda kwao na kuwapoza. Huenda vilevile wakawa na haja juu ya ujio wake. Kwa hivyo ni sawa kufanya hivo kwa sababu kitendo hicho ni utiifu na wema na sio maovu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/367-368)
  • Imechapishwa: 05/01/2020