Kusafiri kwa ndege kwa baba aliye mgonjwa

Swali: Mimi naishi katika nchi hii iliyobarikiwa pamoja na mume wangu. Nataka kusafiri kwa ndege kwenda katika nchi yangu peke yangu kwa sababu baba yangu ni mgonjwa. Mume wangu hawezi kusafiri pamoja na mimi kutokana na shughuli zake. Je, inajuzu kwangu kusafiri peke yangu?

Jibu: Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Hili ni lenye kuenea na linahusu ndege, gari, kipando cha mnyama na kwa miguu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20%D9%85%D9%86%20%D9%85%D8%B5%D8%A7%D9%8A%D8%AF%20%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%B7%D8%A7%D9%86-01-07-1439.lite__0.mp3
  • Imechapishwa: 06/10/2018