Kusafiri katika mji wa kikafiri kwa ajili ya kufanya kazi

Swali: Umesema kuwa haijuzu kusafiri kwenda katika miji ya kikafiri kwa lengo la utalii. Je, inajuzu kwa mtu kusafiri kwenda katika miji ya makafiri kwa ajili ya kufanyakazi na kutafuta riziki huko kwa miaka mingi?

Jibu: Ndio, inajuzu. Ikiwa hakupata kazi katika mji wa Kiislamu, inafaa kwake kusafiri na kutafuta riziki hata kama itakuwa ni katika mji wa kikafiri kwa sharti ashikamane na dini yake. Akipata kazi katika mji wa Kiislamu, haifai akasafiri kwenda katika mji wa kikafiri kwa ajili ya kufanyakazi huko.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (35) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20-%208%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017