Kusafiri katika miji ya Kiislamu kwa ajili ya kutalii

Swali: Mimi ni kijana ambaye nataka kwenda katika mji wa Kiislamu kwa ajili ya kutalii na nataka kwenda pamoja na mke wangu. Ni jambo linalotambulika kwamba utaratibu wa pasipoti wanataka picha ya ndoa. Je, inajuzu kwangu kufanya hivo?

Jibu: Allaah akujaze kheri. Ni wajibu kwangu kukupa nasaha na ushauri ambayo namwabudu Allaah kwao. Namwambia kwamba: usende katika miji mingine. Usende katika miji ya Kiislamu, miji ya magharibi wala ya mashariki. Abaki katika mji wake. Hilo lina usalama zaidi juu ya dini yake na kuna ulinzi zaidi kwa mke wake.

Kuhusu masuala ya kuongezeka kwa matumizi au kupunguka yasikubabaishe. Muhimu abaki katika mji kama mji wetu kwa ajili ya kuhifadhi dini yake na familia yake. Akienda katika miji mingine ataona mambo ya maovu waziwazi yakidhihirishwa masokoni; wanawake wenye kujishauwa na mengineyo ambayo sipendi kuyataja hivi sasa.

Kwa hivyo nasaha zangu kwa muulizaji huyu, kwanza namwambia Allaah amjaze kheri. Mimi nimemwambia kile ambacho kinachomuwajibikia. Nataraji atapokea ushauri wangu: asendi nje ya nchi yetu. Matumizi, kupoteza wakati na mielekeo mingine isiyojua yeyote isipokuwa Allaah pekee.

Ni wajibu kwa mtu kuichunga familia yake uchungaji ulio mzuri. Katika nchi yetu – kutokana na vile nilivyosikia – kuna vitu vya kuona vizuri na mambo ya kimaumbile ambayo yanamtosheleza mtu kutohitajia kutoka nje ya nchi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1081
  • Imechapishwa: 27/03/2019