Kusafiri bila Mahram kwa ajili ya kwenda kumtembelea mzazi

Swali: Mwanamke huyu anauliza kama inajuzu kwake kusafiri bila Mahram kwa ajili ya kwenda kumtembelea mama yake anayeishi katika mji wa kikafiri kwa kuzingatia ya kwamba mama yake hana mtu mwengine huko?

Jibu: Haijuzu kwake kusafiri pasi na kuwa na Mahram. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (68) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/27-06-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 16/07/2017