Kurusha mawe masiku ya Tashriyq inatakiwa iwe baada jua kupindukia

Swali: Inajuzu kutupa mawe tarehe 13 Dhul-Hijjah, siku ya Tashriyq, kabla ya jua kupindukia na kukawa kuna hukumu maalum kwa ajili ya siku hii?

Jibu: Kuna wanachuoni ambao wanaonelea hivo. Hata hivyo dalili zinasema kuwa mtu anatakiwa kurusha mawe baada ya jua kupindukia kisha ndio aende zake. Huu ndio mwongozo wa kinabii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (72) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighassat%20-11-01-1439h.mp3
  • Imechapishwa: 17/12/2017