Kurudisha nia ya swawm baada ya kuikata

Swali: Kuna mtu ni msafiri amenuia kukata swawm yake lakini akawa hakupata chakula. Wakati ilipokuwa karibu na kuzama jua akarudisha nia yake ya kutokula. Ni ipi hukumu ya swawm yake?

Jibu: Haisihi. Kwa kuwa aliponuia kukata swawm yake ilikatika. Haijalishi kitu hata kama hakula na kunywa. Midhali amenuia kukata swawm, imekatika. Akirudisha nia yake haishi kwa sababu swawm ya faradhi ni lazima mtu kutia nia kabla ya kuingia Fajr.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 01
  • Imechapishwa: 23/09/2020