Kurudi nyuma kwenye kiungo alichosahau mtu kukiosha katika wudhuu´

Swali: Wakati nilipokuwa natawadha wudhuu´ wa swalah nilisahau kuosha uso wangu na nikaosha mikono yangu. Baadaye nikakumbuka hilo ambapo nikaosha uso wangu, kisha mikono yangu halafu nikakamilisha wudhuu´ wangu. Je, kuna kitu juu yangu? Ni kipi alichonacho mtu ataposahau kuosha uso wake na asikumbuke isipokuwa baada ya kumaliza kutawadha?

Jibu: Hakuna chochote juu yako. Kwa sababu ulirejea nyuma ukaosha uso wako, kisha mikono yako halafu ukakamilisha wudhuu´ wako. Kuhusu atakayeacha uso wake na asikumbuke isipokuwa baada ya kumaliza kutawadha, basi anatakiwa kurudi kutawadha upya kutokana na ulazima wa kupangilia na Muwaalaah[1].

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/06-faradhi-za-wudhuu/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/102)
  • Imechapishwa: 14/08/2021