Kurudi kwa ajili ya kulingania


Swali: Kuna mtu amehajiri kutoka katika nchi ya kikafiri na kwenda katika nchi ya Kiislamu. Katika ile nchi ya Kiislamu akajifunza misingi ya kidini. Je, inafaa kwake kurejea katika ile nchi ya kikafiri kwa ajili ya kulingania kwa Allaah?

Jibu: Kama anastahiki kulingania na amekuwa na elimu na uwezo basi arudi. Kulingania kwa Allaah ni lengo tukufu. Arudi kwa ajili ya kulingania katika dini ya Allaah kwa sharti awe na elimu, umaizi na utambuzi wa misingi ya ulinganizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ad-Durr an-Nadhwiyd (4) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13474
  • Imechapishwa: 07/02/2021