Kurudi kutoka Hijrah ni dhambi kubwa

Swali: Mtu aliyehama kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu. Baadaye akalazimika kurudi katika mji huo wa kikafiri na kuishi ndani yake. Amefanya dhambi kubwa?

Jibu: Hapana. Ni sawa ikiwa amelazimika kurudi katika mji wa kikafiri. Lakini hatakiwi kurudi ikiwa sio dharurah. Kurudi kutoka katika kuhajiri ni dhambi kubwa. Inahuzu mtu anayerudi jangwani baada ya kujua hukumu za kuhajiri na hukumu za dini. Jangwani kuna mambo ya kutostaarabika. Miji ya kikafiri ni mibaya zaidi kuliko jangwani. Kwa hiyo asirudi huko. Lakini hata hivyo inafaa ikiwa anaenda na kurudi kwa ajili ya biashara, kujitibisha na kuwatembelea ndugu. Hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (68) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/27-06-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 16/07/2017