Kurudi kuswali tena na mkusanyiko baada ya kuswali peke yake


Swali: Nimeswali ´Aswr, Maghrib au ´Ishaa mwanzo hadi mwisho kivyangu kisha baadaye nikapata mkusanyiko – je, niswali pamoja na mkusanyiko na ile swalah ya kwanza iwe faradhi au sunnah?

Jibu: Mtu akiswali faradhi yake kivyake kisha kukahudhuria mkusanyiko baada ya kumaliza faradhi yake, amekwishatimiza faradhi kwa ile swalah yake ya kwanza. Lakini imependekezwa kuirudi swalah yake pamoja na kundi la watu hawa waliofika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkiswali majumbani mwenu kisha mkaja msikitini na mkakuta wanaswali mkusanyiko, basi mswali pamoja nao. Hakika kwenu itakuwa ni naafilah.”

Kujengea juu ya hili tunasema kuwa irudi swalah yako pamoja na wafikaji hawa. Swalah yako hii ya pili itakuwa ni sunnah. Ile swalah ya kwanza ndio faradhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (15) http://binothaimeen.net/content/6794
  • Imechapishwa: 12/02/2021