Kurudi kuswali nyumbani au aende msikitini baada ya kuchelewa?


Swali: Mwenye kuchelewa swalah kwa sababu ya kulala au msongamano wa trafiki bora kwake ni kuswali nyumbani kwake au msikitini?

Jibu: Kama msikitini atapata mtu wa kuswali naye ni vizuri. Ama ikiwa mkusanyiko msikitini umeisha na wala hakuna yeyote basi aswali nyumbani kwake. Katika hali hii sio lazima aende msikitini. Pengine msikiti uko mbali na ikawa ni vigumu kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Maajiyd (54) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16490
  • Imechapishwa: 16/09/2017