Swali: Je, kurejea kwa wanachuoni wakati wa mnasaba wa tofauti au kutaka kutatua tofauti inazingatiwa kuwa ni kufuata kichwa mchunga? Baadhi ya washabiki wanasema kuwa huku ni kuwaabudu wanachuoni.

Jibu: Tazama njama hizi! Wanaita mambo kwa yasiyokuwa majina yake. Wanasema kuwa kurejea kwa wanachuoni ni kuwaabudu. Lakini kurejea kwa al-Hajuuriy sio ´ibaadah? Ni njama na kampeni. Kurejea kwa wanachuoni ni kufuata kichwa mchunga na kurejea kwa al-Hajuuriy sio kufuata kichwa mchunga. Hizi ni njama. Sikuwa nataraji kwa watu wenye kujinasibisha na Sunnah na Salafiyyah kushuka kiasi hicho. Anajipima hali yake kwa kipimo na wengine kwa kipimo kingine.

Kurejea kwa wanachuoni sio kuwaabudu. Wakirejelewa wanachuoni wanaofuata Qur-aan na Sunnah sio kuwaabudu. Ni kumuabudu Allaah. Kwa sababu Allaah ndio Ameamrisha hilo:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Basi ulizeni watu watu wenye Ukumbusho ikiwa hamjui.” (16:43)

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا

”Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza na lau wangelirudisha kwa Mtume na kwa wenye madaraka kati yao, basi wale wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua. Na lau si fadhilah ya Allaah juu yenu na rehema Zake kwa hakika mngelimfuata shaytwaan isipokuwa wachache tu.” (04:83)

Ni Allaah ndiye mwenye kuabudiwa pindi wanaporejelewa wanachuoni. Wanachuoni ndio wenye kutiiwa. Shari´ah imewapa idhini ya kutiiwa. Allaah amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni njia bora na matokeo mazuri zaidi.” (04:59)

“Hakuna watu waliopotea baada ya uongofu waliokuwemo isipokuwa kwa kuleta majadiliano.”Kwa ajili hiyo isisemwi kuwa wanachuoni wanaabudiwa wakati wanaporejelewa. Hakuna anayesema hivo isipokuwa mtu mghafilikaji. Wanachuoni wanaabudiwa pale ambapo wanahalalisha Aliyoharamisha Allaah, wanaharamisha Aliyohalalisha Allaah au wanatunga Shari´ah kwa yale ambayo Allaah Hakuyawekea Shari´ah. Katika hali hii watakuwa wanaabudiwa. Ama kuhusu kuwatii wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah [sauti imepotea], ni utiifu wa Kishari´ah ambao Allaah ameidhinisha bali ameuamrisha. Kurejea kwa wanachuoni sio ufuataji kichwa mchunga wenye kukatazwa. Ni ufuataji wenye kusifiwa. Mnajua watu wanaofuata matamanio na batili wako namna hii. Wana utata. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasoma:

مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ

“Hawakukupigia (mfano huo wa kulinganisha) isipokuwa tu kutaka kujadili. Bali wao ni watu makhasimu.” (43:58)

Ameipokea at-Tirmidhiy kupitia kwa Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) na isnadi yake ni Swahiyh.

Mambo ni hivo. Hakuna watu walipotea baada ya uongofu waliokuwemo isipokuwa ni kwa kuleta majadiliano. Wanaanza kujadiliana, kushikamana na utata na kutokuwa wa wazi:

الْحَمْدُ الله الَّذِي عافاني مِمَّا ابْتَلاك به وفَضَّلني على كَثِيرٍ مِمَّنْ خَلَقَ تَفْضِيلاً

“Ninamshukuru Allaah ambaye amenisalimisha kwa yale aliyowapa mtihani kwayo na akanitukuza mimi juu ya wengi aliyowaumba.”

Ni hadhi kurejea kwa wanachuoni wakati wa mnasaba wa tofauti au wakati wa kutaka kuusitisha, wakati washabiki wa al-Hajuuriy, na kabla yake washabiki wa Abul-Hasan, kwao inachukuliwa kuwa ni kufuata kichwa mchunga. Wanasema:

“Nyinyi mnafuata kichwa mchunga. Huku ni kuwaabudu.”

Wanayaita mambo kinyume na majina yake. Hii ni hadhi kwa watu kuwa nyuma ya wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hii ni hadhi kwa wanafunzi kuwa nyuma ya wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Huenda mtu akasema kuwa ni hadhi pia kuwa shabiki wa al-Hajuuriy au wa Abul-Hasan. Ni hadhi tu pale ambapo mtu anayefuatwa yuko katika njia iliyonyooka na juu ya haki na anafuata Qur-aan na Sunnah na hana makosa. Lakini Abul-Hasan na al-Hajuuriy wana makosa mengi. Hivi sasa wanachuoni wote wanazungumza na wanatahadharisha na mfumo wa Abul-Hasan na al-Hajuuriy. Hivo ndivyo wanavofanya wanachuoni wa Yemen, Misri na Hijaaz. Namna hiyo ndio wanavofanya wanachuoni wote wa Ahl-us-Sunnah ambao wamepitia fitina zote mbili; fitina za Abul-Hasan kwa aina ya Tamyi´ na fitina ya al-Hajuuriy kwa aina ya Haddaadiyyah. Wanachuoni hivi sasa wanatahadharisha fitina hizi mbili. Fitina hizi mbili zinajaribu kuwasonga wanachuoni ili wasirejelewe wanachuoni. Washabiki wa Abul-Hasan marejeleo yao ni Abul-Hasan. Washabiki wa al-Hajuuriy marejeleo yao ni al-Hajuuriy. Wale walio pamoja na wanachuoni wako na wanachuoni wote wanaofuata Tawhiyd na Sunnah na wako na umoja juu ya haki, kheri na uongofu. Wanachuoni hawa wanapambana na msimamo wa ulegezaji na msimamo wa ukali. Msimamo wa ulegezaji ni fitina ya Abul-Hasan na msimamo wa ukali ni fitina ya al-Hajuuriy na fitina ya Haddaadiyyah kabla yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2865
  • Imechapishwa: 11/04/2015