Swali: Mimi ni imamu wa msikiti. Nataka kurefusha swalah ya Tarawiyh na kusoma Qur-aan kwa utaribu na utungo. Lakini wazee nyuma yangu, akiwemo baba yangu, wananikataza kufanya hivo. Wananisomea Hadiyth za kukhafifisha kama mfano wa:

“Je, wewe ni mfitinishaji, ee Mu´aadh?”

na mfano wazo. Ni kipi kidhibiti juu ya idadi ya Tasbiyh na mfano wake katika swalah?

Jibu: Wanachuoni wamesema kuwa idadi ya Tasbiyh katika swalah wingi wake ni kumi na uchache wa ukamilifu wake ni tatu. Lakini tatizo ni vipi tunazisoma Tasbiyh hizo? Baadhi ya watu wanaleta Tasbiyh mbiombio sana. Wanaweza kusoma Tasbiyh nne ndani ya sekunde mbili. Hili si jambo la sawa. Bali unatakiwa kusema:

سبحان ربي الأعلى

“Ametakasika Mola wangu Aliye juu.”

mara tatu.

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

 mara tatu. Hii ndio idadi chache ya ukamilifu. Wingi wake ni mara kumi. Swalah ya Sunnah sio kama swalah ya faradhi. Swalah ya faradhi ni lazima kwa mtu kuhudhuria na kuswali pamoja na mkusanyiko. Ama swalah ya Sunnah sio wajibu. Jengine ni kwamba swalah ya faradhi ni lazima kwa mtu kuswali hali ya kusimama. Lakini swalah ya Sunnah inafaa akaswali hali ya kukaa. Kwa hivyo mwambie baba yako na wazee wenzake wakiwa hawawezi kuswali hali ya kusimama basi waswali hali ya kukaa. Jambo hili ni pana. Wacheni tutumie fursa hii katika mwezi huu uliobarikiwa ili kuzidi kufanya bidii katika matendo mema.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1377
  • Imechapishwa: 26/05/2019