Kurefusha kucha ni kujifananisha na wanyama na makafiri

Swali: Ni ipi hukumu ya kurefusha kucha na kuweka juu yake rangi ya kucha pamoja na kuzingatia kwamba hutawadha kabla ya kuiweka na hukaa masaa 24 kisha naiondosha?

Jibu: Kurefusha kucha ni jambo linaenda kinyume na Sunnah. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Mambo ya kimaumbile ni matano; kutahiri, kutoa nywele za sehemu ya siri, kupunguza masharubu, kukata kucha na kunyofoa nywele za kwapani.”

Haijuzu akaiacha zaidi ya nyusiku arobaini. Imethibiti kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituwekea muda kupungusa masharubu, kukata kucha, kunyofoa nywele za kwapani na kunyoa nywele za sehemu ya siri kwamba tusiache chochote katika hivyo zaidi ya nyusiku arobaini.”

Isitoshe kurefusha kucha mtu anajifananisha na wanyamaa na baadhi ya makafiri.

Kuhusu rangi ya kucha bora ni kuacha kufanya hivo. Ni lazima kuiondosha wakati wa kutawadha kwa sababu inazuia maji kufika kwenye kucha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/49)
  • Imechapishwa: 07/08/2021