Kuraddi utata naosambazwa kwamba Uislamu umeenea kwa upanga

Swali: Unasemaje juu ya mwenye kusema kwamba Uislamu umeenea kwa upanga?

Jibu: Maneno haya kwa kuachia namna hii ni makosa. Uislamu umeenea kwa kulingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall) na pia kwa upanga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilingania Makkah kwa miaka kumi na tatu, kisha vivyo hivyo Madiynah kabla ya kuamrishwa kuanza kupigana vita. Maswahabah na waislamu walienea ulimwenguni na wakalingania katika dini ya Allaah. Na yule ambaye alikuwa akikataa basi walikuwa wakipambana naye. Kwa sababu upanga ni kutekelezeka. Amesema (Ta´ala):

وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ

“Tukateremsha chuma chenye nguvu na manufaa kwa watu.”[1]

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ

“Na piganeni nao mpaka kusiweko shirki na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah.”[3]

Mwenye kukataa wanapambana naye kwa sababu ya manufaa na kufaulu kwake. Ni kama ambavo ni lazima kumtenza nguvu ambaye yuko na haki ya kiumbe mwingine kuitekeleza haki ambayo inamlazimu ijapo ni kwa kutiwa gerezani au kupigwa. Mwenye kufanya hivo hahesabiki ni mwenye kudhulumu. Ni vipi basi kutapingwa au kushangaa kuwalazimisha viumbe wenye haki ya Allaah kuitekeleza? Kusemweje juu ya haki kubwa na ambayo ni ya wajibu zaidi ambayo ni kumpwekesha Allaah (Subhaanah) na kumtoshirikisha?

Miongoni mwa rehema za Allaah ni kule kuweka Kwake (Subhaanah) Jihaad dhidi ya washirikina na kupambana nao ili waweze kumwabudu Allaah pekee na waache kuabudia mwengine asiyekuwa Yeye? Katika hayo ndio kuna ukombozi na kufaulu kwao duniani na Aakhirah.

[1] 57:25

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/277)
  • Imechapishwa: 20/02/2021