Kupwekesha jumatatu au alkhamisi kwa ajili ya swawm

Swali: Inajuzu kupwekesha siku ya jumatatu peke yake kwa kufunga pasi na alkhamisi?

Jibu: Ndio, hakuna neno kupwekesha siku ya jumatatu au alkhamisi. Kinachokatazwa ni kupwekesha siku ya ijumaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msikhusishe usiku wa ijumaa kwa kusimama kati ya nyusiku zengine wala michana yake kwa kufunga kati ya michana mingine.”

Afunge ima siku ya alkhamisi au siku ya jumamosi pamoja na ijumaa. Ama kupwekesha siku ya ijumaa ni jambo limekatazwa. Lakini hakuna ubaya kupwekesha siku ya jumatatu, alkhamisi au jumanne. Kilichokatazwa tu ni kupwekesha siku ya ijumaa. Lakini ikikutana na siku aliyozowea kufunga hakuna neno katika hali hii. Kwa sababu haya ni mazowea yake ya kufunga siku moja na kuacha siku ya kufuatia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 22/09/2018