Swali: Je, inafaa kuzipunguza ndevu…

Jibu: Ndevu sio nzito. Kwa hivyo hazihitajii kupunguzwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuziacha, kuzirefusha, kuzifuga na kuzikirimu. Sio nzito mpaka eti uzipunguze uzito. Hatujaona mtu ambaye alilemewa au kuanguka kwa sababu ya ndevu zake. Hatujapatapo kuona kitu hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 02/05/2021