Kupulizia manukato katika kumbi za ndoa na za mikutano

Swali: Siku hizi kumekithiri walima katika minasana ya ndoa na mengineyo. Baadhi ya watu wanachupa mpaka katika ununuzi wa vitu vyenye kuleta harufu nzuri – au kwa msemo mwingine manukato – ambapo wanatoa kiwango cha pesa kikubwa. Wanaponasihiwa juu ya hilo wanatumia dalili yale yaliyopokelewa kutoka kwa ´Umar pale aliposema:

“Lau mtu atatoa mali yake yote kwa ajili ya kununua vitu vyenye harufu nzuri hazozingatiwa kuwa ni mwenye kufanya israfu.”

Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba manukato ni kitu chenye kupendeza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimependekezewa katika dunia yenu wanawake na manukato. Burudisho la macho yangu imefanywa katika swalah.”

Uhakika wa mambo ni kwamba endapo manukato hayatovuka kile kiwango chake cha kawaida kutakuwa hakuna israfu. Kwa mfano lau sehemu hii kutakuwa kumejaa watu wengi. Kila watu wanavyozidi kujaa, kunapuliziwa manukato. Hii sio israfu. Japokuwa manukato haya kwa nisba ya wale wa kwanza waliojaa itakuwa ni jambo lililokariri. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba sio israfu kwa sababu manukato ya mwisho ni kwa nisba ya wale waliokuja nyuma. Katika hali hii sio israfu. Ama mwenye kuleta manukato mengi na akawa anapulizia manukato sehemu yote pasi na haja hapa ndipo itakuwa israfu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/833
  • Imechapishwa: 25/03/2018