Swali: Kuna mtu anafanya kazi kwenye benki ya ribaa ambapo alimtembelea mmoja katika ndugu zake na akawa ameenda na zawadi kukiwemo chakula na mavazi kwa ndugu wake. Ni ipi hukumu kwa ndugu wale kutumia mavazi haya na kula chakula hichi? Je, ni halali kwao au ni haramu kwao?

Jibu: Inafaa kwao kukila. Kwa sababu yule mwenye kuchuma mali katika njia ya haramu, na mali hiyo ikawa sio haramu kwa dhati yake, inajuzu kwa yule mwenye kuipokea kutoka kwake kwa njia inayokubalika katika Shari´ah kuila. Watu hawa wameipokea kwa njia inayokubalika katika Shari´ah, nayo ni kupokea zawadi. Lakini ikiwa kule kukataa kwao kuipokea zawadi zake itakuwa ni sababu ya kupelekea kujiepusha na ribaa basi katika hali hii itakuwa ni wajibu kwao kuikataa na kumuwekea wazi ya kwamba wamekataa zawadi zake kwa sababu anashirikiana na mambo ya ribaa na kwamba wataipokea mpaka pale atapotubia. Ama ikiwa kufanya hivo hakutomnasua kwa yale anayofanya basi hakuna neno kukubali zawadi zake.

Sisi tunajua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokea zawadi kutoka kwa mayahudi[1]. Katika Khaybar alikubali zawadi ya mwanamke ambaye alimletea nyama ya kondoo. al-Madiynah kuna kijana wa kiyahudi alimwalika mkate wa shayiri na nyama ambapo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaitikia mwaliko wake. Vilevile kuna myahudi alikuwa akinunua chakula kwa ajili ya familia yake na akaweka rehani ngao ya vita kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo alikufa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ngao yake myahudi huu iko kwake.

Kujengea juu ya haya tunawaambia watu hawa ikiwa kule kukataa zawadi zake kutamfanya kuacha kuendelea kushirikiana na mambo haya ya ribaa basi kataeni kuipokea. Ikiwa hakumfanyi hivo na kwamba mtu huyo hatojali kule kurudisha au kutokubali kwenu basi ni sawa kupokea zawadi hizi.

[1] https://firqatunnajia.com/kuitika-mwaliko-wa-chakula-wa-ndugu-ambaye-anakula-ribaa/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/731
  • Imechapishwa: 25/11/2017