Swali: Vipi tutaamiliane na majirani ambao ni manaswara? Je, wakituletea zawadi tuzipokee? Je, inajuzu kwetu kuwaonyesha nyuso zetu au wakaona zaidi ya uso? Je, inajuzu kwetu kununua kwa wauzaji ambao ni manaswara?

Jibu: Mtendee wema yule mwenye kukutendea wema katika wao hata kama atakuwa ni mnaswara. Akikuletea zawadi ambayo inaruhusiwa mtendee wema kwa zawadi hiyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikubali zawadi kutoka kwa kiongozi wa Roma ilihali ni mnaswara. Vilevile alikubali zawadi kutoka kwa mayahudi. Amesema (Ta´ala):

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ

“Allaah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allaah anapenda wafanyao uadilifu.” (60:08)

Inajuzu kwako [mwanamke] kudhihirisha mbele ya wanawake wao [wa kinaswara] yale ambayo inajuzu kuyaonesha mbele ya wanawake wa Kiislamu katika yale yanayofichwa, mavazi ya mapambo na mfano wa hayo. Hii ndio kauli sahihi zaidi ya wanachuoni. Pia inajuzu kununua kutoka kwao vile mnavyohitajia miongoni mwa vitu vinavyoruhusiwa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/303-304)
  • Imechapishwa: 23/08/2020