Kupitwa na swalah ya mkusanyiko kwa ajili ya masomo

Swali: Mimi ni mwanafunzi ninayesoma katika masomo na nina miaka ishirini. Nasoma nje ya mji wangu ambapo nilikulia. Masomo yanaisha nusu saa baada ya swalah ya Dhuhr. Je, inafaa kwangu kuchelewesha swalah ya mkusanyiko na mimi niko masomoni?

Jibu: Swalah ya mkusanyiko ni wajibu kwa mtu isipokuwa ikiwa kama anadhurika katika maisha yake ya kila siku anayohitajia. Ikiwa anapatwa na madhara kwa kutoka klasini kwa ajili ya kwenda kuswali pamoja na mkusanyiko basi hakuna neno akabaki klasini. Ikiwa hapatwi na madhara basi ni lazima kuswali pamoja na mkusanyiko. Ikiwa yeye pamoja na marafiki zake wanaweza kuswali mkusanyiko baada ya kumalizika masomo basi hili ni sahali na jepesi. Kwa sababu wanachuoni wengi wanaona kuwa swalah ya mkusanyiko si lazima kuiswali misikitini. Pamoja na kwamba maoni yenye nguvu ni kwamba swalah ya mkusanyiko ni lazima kuiswali misikitini iliyoandaliwa kwa ajili yake. Huo ndio mwenendo wa wema waliotangulia katika Maswahabah na Taabi´uun.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (11) http://binothaimeen.net/content/6752
  • Imechapishwa: 29/11/2020