Kupeana viungo vya mwili baada ya kufa

Swali: Inajuzu kwa mtu kupeana viungo vyake vya mwili baada ya kufa ili vipandikizwe kwa mtu mwengine?

Jibu: Baada ya kufa haimiliki nafsi yake. Kwa hivyo hawezi kupeana kitu baada ya kufa. Lakini midhali bado yuhai inafaa kwake kupeana viungo vyake ikiwa hadhuriki kwa kufanya hivo na itamfaa yule mgonjwa anayepewa.  Ni lazima kupatikane masharti haya mawili:

1- Kiungo hicho kimfae yule mgonjwa.

2- Mpeaji asidhurike kwa kupeana kiungo hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (59) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-29-01-1438_0.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2017