Swali: Inajuzu kwa mtu akaacha wasia vitolewe viungo vyake baada ya kufa?

Jibu: Hapana. Viungo sio mali yake anayoiachia wasia baada ya kufa kwake. Haijuzu kufanya hivi. Hata hivyo ni sawa kwa aliye hai kupeana kiungo ikiwa hadhuriki kwa kufanya hivo na hilo likawa linamnufaisha yule mgonjwa. Haijuzu kuchukua viungo vya maiti. Atolewe viungo kama gari? Haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (68) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/27-06-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 16/07/2017