Swali: Mtu akitawadha kwa ajili ya swalah na njiani akakutana na myahudi au mnaswara na wakapeana mikono – je, wudhuu´ wake unachenguka? Ni ipi hukumu akimwalika mnaswara kuja kula chakula kwenye nyumba ya muislamu?

Jibu: Muislamu akimpa mkono mnaswara, myahudi au makafiri wengine wudhuu´ hauchenguki. Lakini haifai kwake kupeana nao mikono na wala asianze kumsalimia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msianze kuwatolea salamu mayahudi wala manaswara.”

Kupeana nao mikono ni kubaya zaidi kuliko kuanza kuwatolea salamu. Kwa hivyo asiwaanze na wala asipeane nao mikono. Isipokuwa ikiwa wao wataanza kusalimia na wakanyoosha mikono. Basi katika hali hiyo hapana neno kujibu kwa sababu si yeye ndiye kaanza wao ndio wameanza.

Kuhusu kuwaalika kwenye karamu na kuchangia nao chakula kunahitajia upambanuzi:

1 – Hapana neno ikiwa amewaalika kwa ajili ya kuwapendezesha Uislamu, kuwanasihi na kuwaelekeza katika Uislamu. Vivyo hivyo wakiwa ni wageni.

2 – Kuhusu kuwaalika katika chakula kwa ajili ya urafiki na kuliwazika nao haitakikani kwake kufanya hivo. Kati yetu sisi na wao upo uadui na chuki. Amesema (Ta´ala):

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُ مُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ

”Kwa hakika mna kigezo chema kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga mbali nanyi na yale yote mnayoyaabudu badala ya Allaah. Tunakukanusheni na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha ya milele mpaka mumuamini Allaah pekee.”[1]

[1] 60:04

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/155)
  • Imechapishwa: 25/08/2021