Swali: Akitawadha mtu kwa ajili ya Swalah, na njiani akakutana na mnaswara au myahudi na wakapeana mikono. Je, Wudhuu wake unatenguka? Na ipi hukumu kuwaalika manaswara kula chakula katika nyumba ya Muislamu?

Jibu: Akipeana mikono na manaswara au mayahudi na makafiri wengine atakaokutana nao, Wudhuu hautenguki. Atabaki na Twahara yake. Lakini haifai kwake kupeana nao mikono wala kuanza yeye kuwaongelesha. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Msianze kuwapa mayahudi wala manaswara Salaam.” Na kupeana mikono ni baya zaidi. Tusemeje kupeana nao mikono? Asianze kuwapa Salaam wala kupeana nao mikono. Lakini, wao wakianza kutoa Salaam na kukupa mkono, hakuna ubaya kumjibu. Ama yeye kuanza, hapana asianze. Ama kuwaalika katika walima na kula chakula, hili linahitajia ufafanuzi. Ikiwa malengo ni kutaka kumkaribisha katika Uislamu, kumpa nasaha na kumlingania katika Uislamu, hili halina neno. Ama kumualika katika chakula kwa ajili ya Swadaqah na urafiki, hapana. Kwa kuwa baina yetu sisi (Waislamu) na wao kuna uadui na chuki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 24/03/2018