Kupeana mkono kwa kizushi

Nataka kuwakumbusha baadhi ya ndugu walioko hapa. Walipongia ndani walikuwa wakimpa mkono kila mmoja ambaye ameketi chini. Walikuwa wakimsalimia kila mmoja na kumpa mkono. Kile ninachotaka kuwakumbusha – na ukumbusho ni wenye kuwafaa waumini – ni kwamba Sunnah kwa yule aliyeingia katika kikao cha watu basi ni yeye kutoa salamu ya jumla kwa wale walioko pale. Pamoja na hilo ikiwa ni rahisi kwake kupeana mkono na kila mmoja, basi ni jambo zuri. Isipokuwa rahisi kwake kama kwa mfano ni mkusanyiko wa watu wengi, basi katika hali hiyo atatosheka na kule kutoa salamu. Ama akitoa salamu na kupeana mkono na kila mmoja ambaye ameketi chini si katika Sunnah. Hiyo ni Bid´ah ya kisasa. Zile karne za kale hawakuwa wakiitambua. Na simaanishi zile karne za mwanzo peke yake bali hata zile karne za wale waliokuja nyuma. Kupeana mkono wa mtindo huu ni jambo halitambuliki isipokuwa katika wakati wa sasa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (836) Dakika: 2:05
  • Imechapishwa: 02/01/2021