Kupeana mikono na kukumbatiana baada ya swalah ya ´Iyd

Swali: Ni ipi hukumu ya kupeana mikono, kukumbatiana na kupeana hongera baada ya swalah ya ´Iyd?

Jibu: Mambo haya hayana neno. Kwa sababu watu hawayachukulii kwa njia ya kuabudu na kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall). Wanayachukulia kwa njia ya desturi, ikramu na heshima. Midhali ni desturi hakuna katika Shari´ah kitu kinachoyakataza hayo. Msingi katika jambo hilo ni kuruhusu. Kama ilivosemwa:

الأصل في الأشياء حل ومنع عبادة إلا بإذن الشارع

“Msingi katika mambo ni uhalali na katika ´ibaadah kukomeka isipokuwa kwa idhini kutoka katika Shari´ah.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/209)
  • Imechapishwa: 14/06/2018