Kupeana mikono na kikongwe


Swali: Inaruhusu kwa mwanaume ajinabi kupeana mikono na mwanamke ambaye ni mzee kiasi cha kwamba hana tena matumaini wala hamu ya kuolewa?

Jibu: Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akipeana mikono na wanawake. Bali walikuwa wakimpa kiapo cha usiku na utiifu kwa kuongea tu. Hakuwahi kamwe kugusa mkono wa mwanamke ambaye si halali kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (90) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20-15-07-1439.lite__0_0.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2018