Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

11- Abu Muhammad al-Hasan bin ‘Aliy bin Abiy Twaalib mjukuu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kipenzi chao (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Nilihifadhi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yafuatayo: “Wacha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka.”

Katika mambo ya ´ibaadah kunakuja yakini. Akiingiliwa na shaka asiache yakini yake kwa sababu ya shaka aliyoipata. Kwa sababu yakini haiimtii shaka na ile shaka aliyotumbukia ndani ndio inayomtia shaka na hakinaiki nayo. Kwa mfano akitatizika ndani ya Swalah kama Wudhuu wake umetenguka au hapana? Anachotakiwa ni kujengea juu ya asli: nayo ni ile isiyomtia shaka. Kwa kuwa ameingia ndani ya swalah akiwa na twahara na ni mwenye yakini juu ya hilo. Hivyo ajengee juu ya asli na aachane na shaka iliyomwingilia na kwenda kwenye yakini.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 204-205
  • Imechapishwa: 15/05/2020