Kupata ajira baada ya kughushi


Swali: Inatokea wakati fulani mtu anafanya ghush katika somo kwenye chuo kikuu na kupitia shahada hiyo anapata kazi ya serikali. Unatunasihi vipi?

Jibu: Kumeulizwa sana juu ya hilo. Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) aliulizwa juu ya hilo. Tuliyofikia mimi na Shaykh ni kuwa ikiwa mtu ni mwenye kuiimarisha kazi yake na kufanya kazi yake inavyotakikana, atubu kwa ghush na aendelee na kazi yake. Hana jengine la kufanya zaidi ya hili. Ama akiwa ni lezi kazini shahada haimfai chochote. Haijuzu kwake kusimamia kazi ambayo ni lezi kwayo. Ikiwa ni mwenye kuiimarisha kazi yake hatujali shahada; tunachojali ni kazi yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-09.mp3
  • Imechapishwa: 24/05/2018