Kupangusa shingo wakati wa wudhuu´


Swali: Je, imewekwa katika Shari´ah kupangusa shingo wakati wa kupangusa kichwa wakati wa kutawadha?

Jibu: Haifai. Hii ni Bid´ah. Kupangusa shingo ni Bid´ah:

وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ

“… na panguseni vichwa vyenu na [osheni] miguu yenu… “ (05:03)

Hakusema:

وَامْسَحُواْ بِرُؤُوسِكُمْ

“… na panguseni vichwa vyenu.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha namna ya kupangusa; kuweka mikono miwili iliyolowa maji kuanzia kwenye maoteo ya nywele, kisha unaivuta mpaka nyuma kwenye shingo kisha unarudi tena mwanzo kwenye maoteo ya nywele.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (70) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighatsah%20-%2019%20-0%207%20-%201438.mp3
  • Imechapishwa: 14/10/2018