Kupanga ´Umrah Baada Ya Matembezi Ya Juddah

Swali: Kuna mtu anataka kwenda Juddah kumtembelea mgonjwa. Anafikiria kufanya ´Umrah endapo atapata fursa. Atahirimia wapi huyu?

Jibu: Atahirimia pale atapoazimia kufanya ´Umrah. Inaweza kuwa Juddah, inaweza kuwa nje ya Haram. Atahirimia pale atapoazimia kufanya ´Umrah. Ndio miqati yake. Hivyo ndivyo alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipotaja miqati mbalimbali:

“Atayekuwa mbali na wao afanye hivo pale ataponuia.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 01/01/2017