Kuota wakati wa kufunga na nasaha kwa wenye kukesha nyusiku za Ramadhaan

Swali 424: Mwenye kuota ilihali amefunga swawm yake ni sahihi?

Jibu: Ndio, funga yake ni sahihi. Hakika kuota hakufunguzi swawm. Kwa sababu mtu hakufanya kwa kutaka kwake mwenyewe. Kalamu imenyanyuliwa kwake katika hali ya kulala kwake.

Katika mnasaba huu napenda vilevile kuzindua yale yanayofanywa na baadhi ya watu katika wakati huu ambapo watu wengi wanakesha nyusiku za Ramadhaan. Pengine wanakesha juu ya jambo linalowadhuru na haliwanufaishi. Kisha wanatumia mchana wao wote kulala. Hili ni jambo lisilotakikana. Kinachotakikana ni kwamba mtu aifanye funga yake kuwa ni sehemu ya utiifu, Adhkaar, kusoma Qur-aan na mengineyo katika mambo yanayomkurubisha kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 480
  • Imechapishwa: 11/05/2019