Swali: Kuna imamu wa msikiti amenambia kwamba kuosha nywele mchana wa Ramadhaan kunaharibu swawm. Sababu ya hilo ni kuwa mizizi ya nywele inaingiza maji. Unajibu vipi?

Jibu: Kuosha nywele mchana wa Ramadhaan wakati mtu amefunga hakufunguzi. Wala maji hayaingii ndani ya kichwa. Maneno haya ni ya makosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akioga hali ya kuwa amefunga.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/254)
  • Imechapishwa: 10/06/2017