Kuosha Nyumba Kwa Mtoto Kupatwa Na Kijicho Au Hasadi


Swali: Baadhi ya watu wanaposhakia au wakijua kuwa mtoto wake amesibiwa na hasadi au kijicho wanaosha milango ya nyumba au mwanzo wa nyumba. Ni jambo ambalo limenitia mashaka. Kitendo hichi kimewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Mambo yote haya ni batili na wala hayajuzu. Mambo haya ni batili na wala hayana asli. Lililowekwa ni kuwa, akijua ya kwamba aliemsibu kwa kijicho ni fulani au akifiria kuwa ni yeye, atamwambia aoge, aoshe uso wake na mikono yake na ampe, Allaah Atamnufaisha kwa hilo. Ama kuosha chini na nyumba, yote haya hayana asli.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=14579
  • Imechapishwa: 20/11/2014