Kuonyesha vidole wakati wa kutaja vidole vya Allaah

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nyoyo za waja ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall).”

Je, kuna tatizo kuashiria vidole wakati wa kutaja Hadiyth hii?

Jibu: Hakuna neno. Lengo ni kufanya maana iweze kufahamika. Hakufanywi hivo kwa sababu ya kufananisha vidole vya viumbe na vidole vya Muumba. Lengo ni kufanya maana iweze kufahamika na kwamba ni vidole vya kihakika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (69) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/12-07-1438i.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2017