Kuongezewa miaka ya kuishi kwa sababu ya kuwaunga ndugu na jamaa

Swali: Mawasiliano endelevu yanazingatiwa ni katika kuunga kizazi?

Jibu: Ndio, kunazingatiwa ni kuwaunga ndugu wote.

Swali: Kuongeza umri kunazingatiwa ni jambo la uhakika? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule anayependa akunjuliwe riziki yake na arufushiwe maisha yake basi aunge kizazi chake.”

Jibu: Ndio, inakuwa hivo. Anaongezewa kwa kubarikiwa na anaongezewa miaka. Pengine jambo hilo lilikuwa limetundikwa. Allaah anaweza kumwandikia mtu miaka mia moja kwa sababu ya kuwaunga jamaa zake, mwingine akaandikiwa miaka thamanini kwa sababu ya kuwaunga jamaa zake na mwingine akaandikiwa miaka sitini kwa sababu ya kuwaunga jamaa zake. Inakuwa ni makadirio yaliyoning´inizwa juu ya sababu hizi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21713/حكم-الواصل-المكافى-ومعنى-زيادة-العمر
  • Imechapishwa: 24/09/2022