Kuongea kwa simu wakati wa Twawaaf

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzungumza kwa simu wakati wa kufanya Twawaaf?

Jibu: Hakuna neno:

“Kufanya Twawaaf kwenye nyumba ni kama swalah mbali na kwamba mnazungumza ndani yake.”[1]

Inafaa kuzungumza ndani yake, lakini mtu asikithirishe maneno pasi na haja.

[1]  Ibn Hibbaan (3836).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (24) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-20-02-1435.mp3
  • Imechapishwa: 27/07/2020