Kuongea kunakofaa wakati wa Khutbah siku ya ijumaa

Swali: Mtu ambaye anazungumza na imamu anakhutubu siku ya ijumaa kwa kumdhukuru Allaah au kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – wakati imamu anapotaja hayo katika Khutbah au akaitikia “Aamiyn” juu ya du´aa, je, hayo yanazingatiwa kuwa ni kuongea wakati wa Khutbah? Ni yepi yaliyowekwa na ambayo hayakuwekwa katika Shari´ah kwa maimamu wakati wa Khutbah?

Jibu: Huku hakuhesabiki ni kuongea. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitupigia mfano kwa maneno yenye kuathiri kwa kusema:

“Ukimwambia rafiki yako siku ya ijumaa “nyamaza” na wakati huohuo imamu akawa anatoa Khutbah, basi umefanya upuuzi.”

Wewe hujamwambia mwenzako. Wewe uko pamoja na Mola wako (´Azza wa Jall). Kukitajwa jina la Allaah katikati ya Khutbah basi watakiwa kusema “Subhaan Allaah”. Akitajwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi unatakiwa kumswalia. Kukitajwa thawabu unatakiwa kumuomba Allaah katika fadhilah Zake. Kukitajwa adhabu unatakiwa kumuomba Allaah ulinzi. Yote haya hayahesabiki ni kuzungumza kulikokatazwa. Lakini ni mambo yamewekwa katika Shari´ah kwa mtu kuyasema? Mi naona kuwa hakuna ubaya kuyasema. Mambo haya yanapelekea moyo wake kuwa hadhiri pamoja na imamu tofauti na akipumbaa. Lakini kwa sharti asimshawishi yule aliyeko pembezoni mwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1553
  • Imechapishwa: 23/02/2020